• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia: Mauzo ya nje nchini Ethiopia yaliongezeka kwa dola milioni 115.6

    (GMT+08:00) 2020-10-27 20:15:23

    Uuzaji nje nchini Ethiopia katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2020 ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliopita, mapato ya kuuza nje yaliongezeka kwa dola milioni 115.6 sawa na asilimia 16 na jumla ya Dola za Marekani milioni 838.6 ilipokewa, kulingana na Wizara ya Biashara na Viwanda (MoTI) .

    Sekta ya madini imepata asilimia 300 ya mpango huo na kutengeneza dola milioni 205. Sekta ya viwanda ilipata asilimia 95 na dola milioni 94, wakati bidhaa za kilimo zilipata asilimia 73 na dola 541, MoTI imesema .

    Inasemekana kuwa Usajili wa bidhaa za usafirishaji na utekelezaji wa mikataba ya kuuza nje imechangia pakubwa katika uboreshaji wa biashara ya kuuza nje.

    Aidha imesema kuanzishwa kwa mfumo wa usajili wa mkataba wenye uwajibikaji kwa mikataba ya kuuza nje kuzuia uhifadhi usiofaa wa bidhaa; imefanya biashara ya bidhaa kuendana zaidi na soko la kimataifa na imesababisha kuboreshwa kwa bei za bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako