Wajasiriamali wanawake wa Kenya sasa wana nafasi ya kushinda Sh1 milioni katika mtaji wa mbegu na kupata mafunzo yaliyofadhiliwa juu ya jinsi ya kuwa wanawake wa biashara wenye mafanikio.
Benki ya Standard Chartered Kenya na kituo cha biashara cha Chuo Kikuu cha Strathmore @iBizAfrica wamezindua mpango wa nne wa Women in Tech ambao wanatafuta wanawake katika teknolojia ili kuendesha biashara zao ndogo na za kati.
Programu hiyo iliyozinduliwa mnamo 2017, imewanufaisha wanawake 30 kupitia mafunzo, kati yao 15 bora walianza kupata Sh1 milioni katika mtaji wa mbegu.
Afisa Mkuu wa oparesheni Standard Chartered Bw Peter Gitau amesema kuwa mafunzo yamewezesha walengwa wa zamani kukuza biashara zao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |