Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema, Jumatatu wiki hii ilimkabidhi mtuhumiwa anayehusiana na mauaji wa kimbari wa Rwanda Félicien Kabuga kwa shirika husika mjini The Hague nchini Uholanzi.
Taarifa iliyotolewa jana na Wizara hiyo imesema, hatua hiyo inatokana na uamuzi wa mfumo wa usimamizi wa kimataifa kuhusu kesi zilizobaki za Mahakama ya Jinai ya Umoja wa Mataifa.
Habari zilisema kuwa, Kabuga mwenye umri wa miaka 84 alikuwa mfanyabiashara wa Rwanda, na katika miaka ya karibuni aliishi nchini Ufaransa akitumia kitambulisho feki. Katika kipindi cha mauaji ya kimbari ya Rwanda, Kabuga alichochea chuki kati ya makabila kwa kutumia radio yake binafsi, na alifadhili vitendo vya mauaji hayo. Kabuga alikamatwa mwezi Mei mwaka huu kwenye kitongoji cha Paris.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |