• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania wanawake kutoka Umoja Mataita UN kuwawesha wanawake wa vijiji kiuchumi na usawa wa kijinsia

    (GMT+08:00) 2020-10-28 18:18:02

    wanawake kutoka Umoja Mataita UN wamesema wanawake 118 wa vijijini katika mikoa ya Shinyanga na Singida wamepangwa kufaidika na Kilimo cha maua na ujasiriamali.

    Mafunzo, kulingana na wanawake hao wa UN, yamewekwa ili kukuza wanawake katika ustawi wa uchumi vijijini.

    Taarifa hiyo ilitolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Vijijini (Oktoba 15) ambayo inaleta uwezeshaji wanawake kiuchumi katika kufikia usawa wa kijinsia ambayo ni sharti la maendeleo ya pamoja na endelevu.

    Taarifa hiyo inazingatia pia kuwawezesha wanawake na wakulima wadogo wa kike 'kwa kuboresha uzalishaji wa maua na thamani ya alizeti na uuzaji wa pamoja.

    Maeneo mengine ni ujuzi wa ujasiriamali na kuimarisha usalama wa umiliki wa ardhi, kushughulikia athari za kiuchumi za muda mfupi na za muda mrefu za janga la Covid-19.

    Ofisi ya Kanda ya Wanawake wa UN ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika inaunga mkono uwezeshaji wanawake kiuchumi katika nchi 13 - ambazo zote zina muktadha, vipaumbele na fursa tofauti.

    .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako