Wakulima wa vitunguu saumu nchini Rwanda wameiomba serikali kuwasaidia,wakisema kuwa ukosefu wa upatikanaji wa masoko unaumiza mapato yao.
Kulingana na takwimu kutoka Bodi ya Kitaifa ya Maendeleo ya Mauzo ya Nje ya Kilimo Rwanda (NAEB) ,nchi hiyo ina wakulima wa vitunguu saumu zaidi ya 13,000,waliowekwa katika makundi 11 ya vyama vya ushirika,wanaozalisha zaidi ya tani 3,000 ya vitunguu saumu kila mwaka.
Zao hilo linauzwa nchini na pia katika soko la nje.
Hata hivyo,ufungwaji wa mipaka na nchi jirani ili kudhibiti usambaaji wa maambukizi ya Covid-19 uliathiri mauzo ya nje ya Rwanda ya zao hilo; na kutokana na hilo,wakulima sasa wanategemea tu soko la ndani.
Wanasema hali hiyo imesababisha kuwa na usambazaji wa ziada wa vitunguu saumu katika soko na kusababisha kushuka kwa bei.
Kilo moja ya vitunguu saumu imeshuka maradufu kutoka kati ya Rwf3,000 na Rwf4,000 hadi kati ya Rwf350 na Rwf700, na kuwaingizia wakulima hasara kubwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |