Wizara ya Fedha nchini Ethiopia imetangaza kuwa maandalizi yanaendelea kubinafsisha viwanda 10 vya sukari.
Wizara hiyo imesisitiza kuwa hayo yatafanyika katika njia ambayo itakuwa na manufaa kwa nchi.
Awamu ya kwanza ya mpango huo inatarajiwa kuhusisha viwanda vya sukari vya Wolikit, Beles I na II, na kiwanda cha sukari cha Kesem.
Wizara hiyo aidha imesema kuwa viwanda vya sukari vya Metehara, Fincha and Wonji vitasalia kumilikiwa na serikali ya Ethiopia kwa sasa.
Mshauri katika Wizara ya Fedha nchini Ethipoia Brook Taye (Ph.D.), amesema mengi yamefanywa katika kubinafsisha 10 kati ya viwanda 13 vya sukari ambavyo vinapatikana nchini humo,na kufikia sasa,Taye alisema tathmini ya kiufundi juu ya msimamo wa sasa wa viwanda hivyo umefanywa pamoja ukuzaji wa mikakati ya soko.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |