• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Israel yazindua mtandao wa biashara nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2020-10-29 19:43:59

    Kundi la wajasiriamali na wafanyabiashara chini ya mwavuli wa Empower Africa wiki hii walizindua jukwaa la mtandao wa kibiashara jijini Kigali,Rwanda.

    Wajasiriamali na wafanyabiashara hao wanasema lengo ni kushirikiana na wenzao wa Rwanda katika sekta mbalimbali za biashara kuendesha ukuaji na mabadiliko ya uchumi barani Afrika.

    Empower Africa,iliyoanzishwa na Ezi Rapaport, mtoto wa mfanyabiashara wa Israel Martin Rapaport,inawezesha uwekezaji na biashara barani Afrika.

    Mmoja wa wanachama wa Empower Africa,Caleb Zipperstein alisema anaishukuru serikali ya Rwanda kwa kuifanya nchi hiyo kuwa wazi kwa wafanyabiashara kuzuru.

    Zipperstein alisema Empower Africa ni jumuiya ya wafanyabiashara wanaoaminika ambayo inataka kuungana na warwanda na waafrika wote kuunda ushirikiano kwa ajili ya biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako