• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miradi ya miundo mbinu ya Dogo Kundu yaathiriwa na maporomoko

    (GMT+08:00) 2020-10-30 19:04:46

    Hatari inaonekana kuwakodolea macho wenyeji wa Mombasa kufuatia kuharibika kwa sehemu za miradi miwili mikubwa ya miundo msingi katika Kaunti hiyo.

    Kamati ya Bunge kuhusu Uchukuzi imesema maporomoko ya ardhi yamesababisha nyufa katika sehemu ya barabara ya pembeni ya Dongo Kundu na mkondo wa ndege kutua na kupaa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi (MIA).

    Akiongea na wanahabari katika uwanja huo, mwenyekiti wa kamati hiyo David Pkosing alisema kuwa miradi hiyo miwili inakabiliwa na hatari ya kuharibika ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa.

    Mwenyekiti huyo alikuwa katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya miundo msingi katika eneo la Pwani.

    Bw Pkosing alisema sehemu za kusini na magharibi mwa uwanja wa ndege wa Moi zinakabiliwa na hatari ya kuharibika licha ya kazi nzuri ambayo inafanywa katika eneo la kaskazini mwa uwanja huo.

    Barabara ya Dongo Kundu iko pembeni mwa mkondo huo wa kutua na kupaa kwa ndege na maji yote ambayo hukusanywa katika uwanja wa MIA, hupenyeza chini ya ardhi yakielekea katika Bahari ya Hindi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako