• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UGANDA: MAPATO YA DHAHABU YAONGEZEKA HADI SHILINGI TRILIONI 5.4

    (GMT+08:00) 2020-11-02 16:59:27

    Licha ya kwamba hakuna ripoti kamili kuhusu uwepo wa madini ya dhahabu nchini Uganda, na haswa ni kiwango chake kote nchini, bidhaa hii muhimu imeingizia taifa la hili jumla ya dola bilioni 1.4 za kimarekani, sawa na shilingi trilioni 5.4, pesa za Uganda kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti.

    Ripoti kutoka Benki Kuu nchini Uganda zinaonyesha kwamba dhahabu ilileta fedha nyingi za kigeni kushinda bidhaa zote zilizouzwa nje kwa kipindi cha mwaka mmoja ulioshia mwezi Agosti mwaka huu. Uganda ilipokea takriban dola milioni 112.7 kila mwezi kutoka kwa mauzo ya dhahabu nje ya taifa.

    Kuanzia Agosti 2019 na Agosti mwaka huu, Uganda ilikusanya jumla ya dola bilioni 1.4, ikiwa ni ongezeko la dola bilioni 900, kutoka dola bilioni 1.2 kipindi kama hicho. Ripoti ya Benki Kuu ya Uganda ikionyesha kwamba, jumla ya kilo 31,490.48 za dhahabu ziliuzwa nje ya taifa katika kipindi cha mwaka mmoja.

    Soko kuu la dhahabu kutoka Uganda ni mataifa ya Mashariki ya Kati, huku milki za Kiarabu zikiongoza kwa ununuzi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako