• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Arsenal yavunja rekodi mbaya mbele ya Man United

    (GMT+08:00) 2020-11-03 17:08:13

    Ni sura za huzuni ndio zimetawala pale katika Jiji la Manchester baada ya Man United kupoteza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Arsenal kwa kipigo cha bao 1-0. Mchezo huo ambao ulianza saa 1:30 unakuwa mchezo wa nne kwa Man United kushindwa na kupata ushindi mbele ya Arsenal. Baada ya mchezo huo kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer alisema kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake kilikuwa cha chini sana na walikuwa wazito kuanzia kwenye kupiga pasi na kutengeneza mashambulizi. Huo unakuwa ni ushindi wa kwanza wa Arsenal kwenye Ligi Kuu katika dimba la Old Trafford baada ya kupita miaka 14. Man United inakuwa imepoteza mchezo wa tatu baada ya kupata kufungwa na Crstal Palace 3-1, Tottenham 6-1. Huku mchezo uliopita dhidi ya Chelsea ikiambulia sare ya 0-0 na kukusanya alama saba katika michezo sita. Kocha wa Arsenal Mikel Arteta alisema miaka 14 bila ya kupata ushindi ni mingi kwake ni faraja kuona ameivunja historia hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako