• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda Yawekeza Rwf15 Bilioni katika Nguruwe, Ufugaji wa Kuku

    (GMT+08:00) 2020-11-03 20:30:56

    Mapato kutoka kwa nguruwe na kuku inatarjiwa kuongezeka baada ya hatua mpya zinazolenga kupunguza bei za malisho ya wanyama na kuboresha ubora wa mifugo.

    Nchi Imewekeza Rwf bilioni 15 kwa mradi ambao ulizinduliwa hivi karibuni na Ushirikiano wa Masoko ya Mifugo midogo (PRISM), ili kukuza mnyororo wa thamani ya mifugo.

    Mradi huo wa miaka 5 pia unatafuta kuvutia uwekezaji wa kibinafsi katika tasnia kupunguza uagizaji wa mayai na nyama. Imefadhiliwa na Wakala wa Maendeleo wa Ubelgiji - mradi huo unatekelezwa kwa kushirikiana na Bodi ya Kilimo ya Rwanda (RAB).

    Matarajio ni kwamba ifikapo mwaka 2023 wanalenga kuwa na wafugaji wa kuku na nguruwe 12,000 na angalau wazalisha 9,000 wa maharagwe na mahindi.

    Kulingana na takwimu kutoka RAB, Rwanda ina idadi ya kuku milioni 5.3 na nguruwe milioni 1.38. Nchi inazalisha wastani wa tani 9,000 za mayai, tani 37,300 za nyama ya kuku, na tani 23,000 za nguruwe kwa mwaka kama 2019.

    Mpango mkuu wa mifugo wa Rwanda unalenga zaidi ya mara mbili ya uzalishaji wa nyama ya nguruwe kutoka tani 67,076 kufikia 2022.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako