Benki ya Dunia itaingiza $1.2 billion (takriban Rwf1.1 trilion) kama sehemu ya mfumo wa nchi ya Rwanda katika kipindi cha kati ya 2021 na 2023.
Mfumo huo wa ushirikiano na fedha zilizoahidiwa na Benki ya Dunia zinatarajiwa kuchukua sehemu kuu katika kuifufua Rwanda kutokana na athari za janga la Corona.
Mfumo huo wa ushirikiano unaonyesha kuwafedha hizo zitatumika katika kuboresha mtaji wa binadamu,uboreshaji wa hali kwa maendeleo ya sekta binafsi,upanuzi wa miundombinu na uchumi wa kidijitali.
Aidha fedha hizo pia zitaenda kuongeza uzalishaji wa kilimo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |