• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wavuvi na wakulima nchini Tanzania wahakikishiwa masoko

    (GMT+08:00) 2020-11-04 18:08:58

    Wakulima na wavuvi katika mikoa sita ya Kanda ya Ziwa nchini Tanzania wamehakikishiwa soko la mazao yao pamoja na samaki wanaovua katika Ziwa Victoria.

    Hayo yamesemwa jana jijini Mwanza na Meneja wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Mike Granta.

    Granta alisema katika kuendeleza kilimo, Benki ya TADB imetoa Sh. bilioni 40 kwa vyama vikuu ya ushirika mkoani Kagera ili kuwaendeleza wakulima.

    Alisema fedha hizo ni kwa ajili ya kununua mazao ya wakulima hao, kupitia ushirika wao ili kuhakikisha kwamba wanakuwa na soko la uhakika.

    Aliongeza kuwa miaka ya nyuma wanunuzi binafsi walikuwa wananunua mazao ya wakulima ikiwamo kahawa kwa bei ndogo, lakini baada ya TADB kutoa fedha hizo kwa vyama vya ushirika, sasa wanalipa bei nzuri.

    Meneja huyo alisema mpaka sasa asilimia kubwa ya kahawa na pamba inauzwa nje ya nchi, na kwamba sehemu kidogo inayobaki inauzwa nchini Tanzania.

    Katika kuhakikisha TADB inaendeleza kilimo, Granta alisema katika Kanda ya Ziwa wametoa mikopo ya matrekta zaidi ya 50 yenye riba nafuu ili kuhakikisha wakulima wanalima kwa tija.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako