Polisi nchini Nigeria imesema imewakamata zaidi ya watu 1,500 kwenye operesheni kubwa ya nchi nzima dhidi ya watu wanaoshukiwa kupora maghala ya serikali yanayohifadhi vitu na kuvamia nyumba za watu na kuchukua vitu vya thamani wakati wa maandamano.
Inspekta jenerali wa polisi Mohammed Adamu amesema jumla ya watuhumiwa 1,590 wamekamatwa kutokana na kuandamana wakipinga ukatili wa polisi, usumbufu na mauaji yanayofanywa na kikosi maalumu cha kupambana na wizi ambacho sasa kimeshavunjwa.
Adamu amebainisha kuwa polisi 22 wameuawa na waandamanaji hao wenye hasira na wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya kwenye maandamano hayo, na kuongeza kuwa vituo 205 vya polisi na miundombinu muhimu binafsi na ya umma pia imeharibiwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |