Kenya na Uingereza zimefikia makubaliano mapya ya biashara, ikiwa imesalia chini ya miezi 2 kabla ya kumalizika kwa manufaa yaliyopo ya ufanyaji biashara kwa Kenya kabla ya Uingereza kuondka rasmi kutoka kwa Umoja wa Ulaya.
Mkataba huo mpya, ambao ni pamoja na vifungu kutoka kwa Makubaliano ya zamani ya Ushirikiano wa Kiuchumi chini ya Jumuiya ya Ulaya, sasa yatafanywa rasmi wakati wa kusaini makubaliano ya pande hizo mbili.
Waziri wa Biashara Betty Maina amesema makubaliano hayo yatatoa mwendelezo kwa wafanyabiashara, wawekezaji na minyororo ya usambazaji na kuweka misingi ya maendeleo zaidi ya uchumi.
Makubaliano hayo yatakuwa na faida kwa uuzahi wa nje wa bidhaa za Kenya kama chai, kahawa, mboga na maua huku nayo Uingereza ikiuza kwa marsti nafuu bidhaa kama magari na madawa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |