Serikali ya Uganda imesema inapoteza ushuru kutokana na kuongezeka kwa uagizaji wa pikipiki kwa njia ya magendo kwenda katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Imesema pikipiki hizo zinapitishwa kwenye ziwa Albert katika wilaya za Hoima, Buliisa, Kagadi na Kikuube.
Mkuu wa mamlaka ya mapato kkatika kanda ya magharibi ya kati bwana Silas Kayumba, amesema zaidi ya pikipiki 20 huuzwa kila mwezi kwa njia ya magendo.
Kwa kila pikipiki serikali inapoteza ushuru wa kati ya dola 130 na dola 200.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |