• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria: Mradi wa Usafishaji wa Petroli ya Dangote kukanza kazi mwaka ujao

    (GMT+08:00) 2020-11-05 19:23:02

    Mradi wa Usafishaji wa Petroli ya Dangote huko Lagos sasa umekamilika kwa asilimia 80 na uzalishaji unatarajiwa kuanza katikati ya mwaka ujao.

    Aidha kiwanda cha mbolea cha dola bilioni 2 cha Dangote chenye uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu za urea na amonia kitaanza uzalishaji mwezi huu.

    Miradi yote iko katika Eneo la Biashara Huria la Lekki mjini Lagos.

    Mkurugenzi Mtendaji wa miradi na Mitaji wa Viwanda vya Dangote Devakumar Edwin amewaambia waandishi wa habari kuwa kiwanda hicho cha kusafisha mafuta kitaajiri zaidi ya watu 240,000.

    Edwin hata hivyo amesema kukamilishwa kwa miradi hiyo kumecheleweshwa na janga la corona na bidhaa nyingi za ujenzi zilikwama nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako