Serikali ya Rwanda inawekeza frac bilioni 15 kwenye miradi ya ufugaji nguruwe na kuku.
Miradi hiyo itatekelezwa ndani ya miaka 5 na itahusisha pia sekta binafsi ili kupunguza uagizaji wa mayai na nyama.
Inafadhiliwa na shirika la Enabel ambalo ni la Maendeleo kutoka Ubelgiji, na utekelezaji utafanywa na halmashauri ya kilimo nchini humo.
Naibu mkurungezi wa Utafiti wa Wanyama na Uhamishaji wa Teknolojia kwenye halmashauri hiyo Solange Uwituze, amesema mwaka 2023 wanalenga kuwa na wafugaji wa kuku na nguruwe 12,000.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |