• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahasibu Tanzania kukutana Novemba 12

    (GMT+08:00) 2020-11-05 19:23:44

    Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) kinatarajia kufanya mkutano wake mkuu wa kawaida wa 37 Novemba 12-13, mwaka huu jijini Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).

    Mwenyekiti wa Chama hicho, CPA. Peter Mwambuja alisema mkuatano huo kwa mwaka huu utakuwa na kaulimbiu ya "Ushiriki wa Wahasibu kwenye Uendelevu wa Uchumi wa Kipato cha Kati Tanzania.

    Alisema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James na kwamba baadhi ya ajenda zitakazojadiliwa ni pamoja na Ripoti ya mwaka ya Baraza la Uongozi, Hesabu zilizokaguliwa za Mwaka wa Fedha uliopita, Mabadiliko ya Katiba ya Chama cha Wahasibu, na menginevo.

    Alisema tukio hilo litakuwa ni jukwaa la wadau mbalimbali wa taaluma hiyo kuonyesha huduma mbalimbali ikiwamo uzoefu huku gharama ya ushiriki ikiwa ni Sh 200,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako