Waganda maskini nchini Uganda wanatarajiwa kufaidika na ujuzi utakaowawezesha kujenga viwanda vido vitakavyoboresha mapato yao na hatimaye kuboresha maisha yao.Hii ni kufuatia kuzinduliwa kwa makubaliano kati ya taasisi ya kutoa mafunzo ya kiufundi chini ya mradi wake wa Pamoja wa thamani ya shilingi milioni 850 ambao unalenga kuwawezesha Waganda wenye maisha ya chini kupata mafunzo ujuzi wa kufanya biashara mbali mbali. Akizungumza na radio China Kimataifa mjini Kampala Uganda,mkuu wa mradi huo Andrew Mwesigye amesema mradi huo pia utapunguza pengo la ukosefu wa ajira nchini Uganda. Mafunzo hayo ni pamoja utengenezaji wa Radio na Televisheni, vifaa vya umeme majumbani, usukaji wa nywele na mitindo ya nguo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |