• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi kuu ya Uingereza yaendelea, kutokuwepo kwa watazamaji bado changamoto

    (GMT+08:00) 2020-11-09 18:33:17

    Wikiendi iliyopita ligi kuu ya England iliendelea na kulikuwa na baadhi ya mambo ya kushangaza. Tottenham wamebahatika kupata ushindi ugenini dhidi ya West Bromwich Albion. Mshambuliaji Harry Kane alifunga goli katika dakika ya 87 na kuwa goli lake la 150 katika ligi hiyo, na kufikisha timu yake katika nafasi ya pili ya ligi. Ulikuwa ni uzembe wa mabeki wa WBA ndio ulimpa nafasi Kane kutingisha nyavu. Kulikuwa na mechi nyingine ambayo ilionekana kama ni mechi ya kukata na shoka kati ya Liverpool na Man City, mechi ambayo kocha wa Liverpool Jurgen Klopp aliitia mechi ngumu. Mechi hiyo iliisha kwa suluhu ya goli moja kwa moja, Gabriel Jesus wa Man City akitingisha nyavu baada ya Mo Salah wa Liverpool kuanza kuwafungia Liverpool.

    Arsenal wameendelea kuwasikitisha mashabiki wao kwa kuchapwa magoli matatu kwa nunge nyumbani na Aston Villa. Kwa sasa kileleni mwa ligi wapo Leicester City, wakiwa na pointi 18 baada ya kuwachapa Wolves nyumbani. Hata hivyo kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya makocha ni ratiba ngumu inayowapa wachezaji muda wa wiki chini ya wiki mbili tu kupumzika. Pep Guadiola amelalamika kuwa LeBron James anapumzika kwa miezi mitatu baada ya kumaliza msimu, lakini wachezaji wa Premier League wana mapumziko mafupi sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako