• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sare ya Simba na Yanga yazua maswali kuhusu mwelekeo wa VPL Tanzania

    (GMT+08:00) 2020-11-09 18:33:37

    Mabingwa watetezi wa ligi ya Tanzania VPL, Simba SC, wamenusurika kupoteza mechi mbele ya watani wa jadi, Yanga SC baada ya kulazimisha sare ya 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Yanga SC inayofundishwa na Mrundi Cedric Kaze inafikisha pointi 24 na kuendelea kushika nafasi ya pili, ikizidiwa pointi moja na Azam FC, wakati Simba SC inabaki nafasi ya tatu ikifikisha pointi 20 baada ya wote kucheza mechi 10. Hadi mapumziko Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Mghana Michael Sarpong kwa mkwaju wa penalti dakika ya 31. Safu ya ulinzi ya Yanga SC ilipata pigo baada ya kumpoteza beki wake tegemeo, Mghana Lamine Moro aliyeumia goti na kushindwa kuendelea na mechi, nafasi yake ikichukuliwa na Said Juma mwanzoni mwa kipindi cha pili. Katika dakika za mwisho Mkenya Onyango aliisawazishia Simba SC kwa kichwa dakika ya 86. Kukamatana huko kwa Simba na Yanga kunafanya Azam iendelee kuwa kileleni, na kuzua maswali kama msimu huu ufalme wa Simba na Yanga kwenye VPL uko kwenye hatihati, na hiyo itakuwa na maana gani kwa soka ya Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako