• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Real Madrid wachapwa magoli manne na kukumbwa na kizunguzungu kingine

    (GMT+08:00) 2020-11-09 18:33:55

    Klabu ya Valencia imewashangaza waspaniola baada ya kuwachapa Real Madrid magoli manne kwa moja, huku Carlos Soler akifunga hat-trick kwa njia ya penalti. Ajabu ni kuwa Madrid ndio walikuwa wa kwanza kutingisha nyavu za Valencia kupitia goli lililofungwa na Karim Benzema. Valencia walisawazisha na baadaye kuendelea na magoli mengine matatu zaidi. Soler ameleta kilio hicho kwa Madrid, si siku nyingi baada ya kuaibishwa na klabu ya Ukraine walipochapwa 3-2. Hiki ni kipigo kikubwa cha pili kwa Real katika msimu huu, na kizito zaidi cha ligi tangu walipofungwa 5-1 na Barcelona mnamo Oktoba 2018. Madrid wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo kwa pointi 16 baada ya michezo minane, wakati Real Sociedad wakiwa kileleni na pointi 20 baada ya michezo tisa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako