• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ZANZIBAR: BODI YA WAUZA VILEO YAWAOMBA WAUZAJI KUFUATA SHERIA MPYA.

    (GMT+08:00) 2020-11-09 19:22:22

    Bodi ya Ushauri na Udhibiti wa vileo Zanzibar, imewataka wafanyabishara wa vileo kuhakikisha wanakamilisha taratibu za maombi, ili kufanyiwa ukaguzi na kupatiwa leseni.

    Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo Abdulrazak Abdulkadir Ali, mara baada ya kufanya ukaguzi kwenye maeneo ya wafanyabiashara na wasambazaji wa vileo ambao wamekamilisha taratibu.

    Alisema lengo la ukaguzi huo ni kutekeleza sheria mpya ya vileo sheria nambari 7, ya mwaka 2020 ambayo inalengo la kudhibiti utitiri wa baa zisizo na leseni na ambazo zinaendeshwa kinyume na sheria.

    Mwenyekiti huyo alisema sheria hiyo imekuja na mabadiliko makubwa hasa kuhusu wapingaji wa baa zilizokaribu na makazi ya watu, ambazo amehakikisha utitiri huo unapungua. Hivyo aliwataka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanakamilisha taratibu hizo kabla ya muda uliowekwa na bodi hiyo kwa sababu zipo hatua kali zilizowekwa kwa ajili ya wale wanaokiuka sheria.

    Akizungumzia kuhusu ukaguzi huo alisema wamebaini kwamba baadhi ya ghala hazina vipozea joto jambo ambalo ni hatari kwa sababu linaweza kuleta athari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako