• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ZANZIBAR: KASI YA WATALII WANAOINGIA ZANZIBAR YAONGEZEKA

    (GMT+08:00) 2020-11-09 19:22:41

    Zaidi ya watalii 500 kutoa Urusi waliingia nchini wiki jana kupitia kiwanja cha ndege cha Abeid Amani Karume, ambapo ni mara ya kwanza Zanzibar kupata watalii idadi kubwa tangu kufunguliwa kwa viwanja vya ndege.

    Watalii hao waliwasili kwa Shirika la Ndege la Azur Air kutoka nchini Urusi, ikiwa na watalii wenye rika tofauti ambao wengi wao ni vijana. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu mtendaji wa kamisheni ya utalii Zanzibar, Dk. Abdallah Mohammed Juma, alisema kuwa licha ya ujio wa wageni hao, lakini pia Zanzibar inatarajia kupokea ndege 100 za watalii ambazo zipo katika foleni ya kuja Zanzibar.

    Alisema kuwa baada ya Tanzania kufanikisha kutokomeza ugonjwa wa korona, utalii umefunguka na hoteli nyingi sasa zitafunguliwa kutokana na watalii wengi kuwasili Zanzibar.

    Aidha alisema uchaguzi Zanzibar umekwisha na hali ya usalama imeimarika ambapo amani iliyokuwepo imekuwa sababu kuu ya watalii wengi kuja humo. Pia alisema kuwa shirika la ndege la Ujerumani kwa mara ya kwanza litaanza safari zake linatarajiwa kuleta ndege yake kubwa kuleta watalii Zanzibar ikitokea moja kwa moja Ujerumani ambayo itawasili Zanzibar Disemba 31 mwaka huu

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako