Mamlaka nchini Rwanda zimefungua tena baadhi ya sehemu za magharibi ya mpaka kati yake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika wilaya ya Rubavu, baada ya kufungwa kwa zaidi ya miezi saba kuanzia mwezi Machi, ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.
Gavana wa mkoa wa Magharibi Alphonse Munyantwari alisema, ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona, wasafiri wanatakiwa kufuata kanuni za kiafya, zikiwa ni pamoja na kufanyiwa vipimo vya kasi vya COVID-19 kabla ya kuruhusiwa kufunga safari. Hatua hii huenda ikaathiri shughuli za kibiashara kati ya mataifa haya mawili .
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |