• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Patrick Motsepe wa Afrika Kusini apanga kuwania Uenyekiti (CAF)

    (GMT+08:00) 2020-11-10 18:17:12

    Mmiliki wa timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Patrick Motsepe, amepanga kuwania Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) katika Uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo utakaofanyika Machi mwakani huko Rabat, Morocco. Uamuzi wa Motsepe kuwania nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa mpira wa miguu Afrika, umetangazwa jana na Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA), Danny Jordaan katika mkutano wake na waandishi wa habari. "Caf inatakiwa kuimarisha nguvu yake duniani. Ni mtu sahihi ambaye tunaweza kumuweka katika uongozi wa Caf. Hatutaki shida yoyote katika utawala na maadili kwenye mpira wa miguu," alisema Jordaan akionekana pia kumpiga kijembe Rais wa sasa wa Caf, Ahmad Ahmad. Kuibuka kwa Motsepe kunamfanya awe mtu wa tatu kuonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo ya Urais wa Caf, akiungana na Rais anayemaliza muda wake, Ahmad na Jacques Anouma aliyewahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako