• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchezaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright asema kiwango cha Arsenal hakiridhi

    (GMT+08:00) 2020-11-10 18:17:29

    Mkongwe wa Arsenal, Ian Wright ameishukia timu yake ya zamani kuwa imeonyesha kiwango kibaya zaidi msimu huu baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa. Vijana wa kocha Mikel Arteta wameshuka hadi nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kutokana na kipigo hicho cha juzi kwenye Uwanja wa Emirates. Ian Wright amesemani kiwango kibovu mno ambacho amewahi kukiona kikionyeshwa na Arsenal. Kocha wa Mikel Arteta aliwapumzisha nyota wake kadhaa kwenye mchezo wa Arsenal wa Ligi ya Europa dhidi ya Molde, Alhamisi, lakini bado walishinda mabao 4-1. Hata hivyo, wachezaji nyota waliopumzishwa katikati ya wiki kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu hawakusaidia timu yao kukwepa kipigo cha nyumbani dhidi ya Aston Villa. Amesema wachezaji walikuwa mbali zaidi ya kiwango walichoonyesha dhidi ya Manchester United. Wakati huo huo, mchezaji mwenzake wa zamani na mchambuzi wa masuala ya soka, Alan Shearer aliwapongeza wachezaji wa Aston Villa kwa kuonyesha soka safi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako