• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbwana Samatta kutojiunga na wenzake Tunisia

    (GMT+08:00) 2020-11-10 18:17:46

    Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachovaana na timu ya Taifa ya Tunisia Novemba 13. Mbwana Samatta ambaye ni mshambuliaji na jina lake lipo kwenye orodha ya wachezaji 27 walioitwa kuunda kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Kwa sasa Stars chini ya Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije imeweka kambi nchini Uturuki ambapo nyota huyo anacheza nchini humo. Habari zinaeleza kuwa Samatta hayupo kwenye mazoezi na timu ya Taifa ya Tanzania kwa kuwa ana matatizo ya kiafya, na ameshauriwa na madaktari kutocheza ili arejee kwenye ubora wake.

    Winga wa Harambee Stars Ayub Timbe Masika ambaye aliichezea timu ya Beijing Renhe ya hapa China, amesema ana imani kuwa Harambee stars itafuzu kwenye michezo ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2021 (Afcon) itakayofanyika nchini Cameroon Januari 2022. Winga huyo anaamini kuwa timu yake ina nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa kwenye mashindano ya 2019 huko Misri. Kesho Kenya inawakaribisha Comoro katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo, na watasafiri kwenda Moroni kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumapili, Novemba 15.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako