• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baada ya ubingwa bara Simba sasa waanza safari ya mechi za kimataifa

    (GMT+08:00) 2020-11-10 18:18:06

    MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wameweka wazi kuwa hesabu zao kubwa kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Msimu uliopita Simba ilipokuwa chini ya Patrick Aussems iliishia hatua ya awali kwa kutolewa na UD Songo kwa faida ya bao la ugenini jambo ambalo lilisababisha kibarua cha kocha huyo ambaye aliifikisha hatua ya robo fainali timu hiyo kuota nyasi. Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa hesabu kubwa kwa sasa ndani ya timu hiyo ni kuweza kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba itakutana na Plateu United ya Nigeria mchezo unaotarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 27-29 na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 4-6 Uwanja wa Mkapa. Droo ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika imefanyika nchini Cairo ambapo kwa Tanzania, Simba inaiwakilisha Tanzania Ligi ya Mabingwa Afika baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita. Mshindi kati ya timu hizo atakunata na mshindi kati ya Costa do Sol ama FC Platinum. Timu ya Sfaxien ya Tunisia itamenyana na Mapinduzi ya Zanzibar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako