• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya tatu ya bidhaa za kimataifa ya China CIIE yafungwa

    (GMT+08:00) 2020-11-10 19:32:38

    Maonesho ya tatu ya bidhaa za kimataifa ya China (CIIE) yamefungwa leo huko Shanghai. Naibu mkurugenzi wa idara ya maonesho hayo Bw. Sun Chenghai, amesema ingawa maambukizi ya virusi vya Corona yanaendelea kuenea kote duniani, nia ya kufanya ushirikiano kwa pande mbalimbali za maonyesho hayo haikupungua. Thamani ya mikataba iliyofikiwa imefikia dola za kimarekani bilioni 72.62, kiasi ambacho kimeongezeka kwa asilimia 2.1 kuliko maonyesho hayo ya mwaka jana.

    Bw. Sun amesema, maonyesho hayo yameonyesha bidhaa mpya, teknolojia mpya na huduma mpya za aina zipatazo 411. Amesema idara kadhaa za China zilitoa sera za kuunga mkono maonyesho hayo ikiwemo kutoza ushuru nafuu, kurahisisha utaratibu wa forodha na idhini ya kuingia kwenye soko, ili kuleta manufaa zaidi kwa wafanyabiashara walioshiriki kwenye maonyesho hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako