• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China ahutubia mkutano wa 20 wa baraza la wakuu wa nchi wanachama wa SCO

    (GMT+08:00) 2020-11-10 19:37:02

    Rais Xi Jinping wa China tarehe 10 jioni amehutubia mkutano wa 20 wa baraza la wakuu wa nchi wanachama wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai SCO kwa njia ya video.

    Rais Xi amesisitiza kuwa kutokana na hali ilivyo sasa, Shirika hilo linatakiwa kueneza "moyo wa Shanghai", kuzidisha mshikamano na ushirikiano, ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya utulivu na maendeleo ya nchi za kanda hiyo, na kufanya juhudi zaidi za kiutendaji kwa ajili ya kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Rais Xi pia amesisitiza kuwa, tunapaswa kuchukua hatua halisi kutekeleza hali yenye pande nyingi, kukamilisha usimamizi wa dunia, na kulinda utaratibu wa kimataifa. Tunapaswa kushikilia kanuni ya kujadiliana, kujenga kwa pamoja na kunufaishana, kutoa mwito kujadili kwa pamoja mambo ya dunia, kujenga kwa pamoja mfumo wa usimamizi na kunufaika pamoja na matokeo ya maendeleo kwa watu wa nchi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako