• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • South Sudan: Benki Kuu Yaanzisha Mabadiliko Ya Fedha Kuokoa Uchumi Unaoumia

    (GMT+08:00) 2020-11-10 19:54:03

    Benki Kuu ya Sudan Kusini imesema itaimarisha sera ya fedha ya nchi hiyo ili kupunguza kupungua kwa kasi kwa Pound ya Sudan Kusini dhidi ya dola ya Kimarekani.

    Katika mkutano wa dharura ulioongozwa na gavana mpya aliyeteuliwa, Dier Tong amesema kamati ya tasisi ya Sera ya Fedha hiyo iliweka maazimio matano yaliyolenga kukabiliana na kushuka kwa thamani.

    Akiwahutubia wanahabari huko Juba, ameonyesha matumaini yake kuwa sera mpya zilizowasilishwa na benki kuu zitapunguza mfumuko wa bei uliopo.

    Miongoni mwa sera zilizokubaliwa na kamati ni nyongeza ya kiwango cha riba ya benki hadi asilimia 15 Kuongezeka kwa kiwango cha mahitaji ya akiba ya benki kwa benki za biashara na uwiano wa akiba ya fedha hadi asilimia 20.

    Sarafu ya nchi hiyo imekuwa ikishuka kwa kiwango kikubwa kufuatia kushuka kwa mapato ya mafuta nchini na kasoro katika ukusanyaji wa mapato yasiyokuwa ya mafuta.

    Wateja wamelalamika juu ya kupanda kwa kasi kwa bei ya bidhaa za kimsingi wakati wafanyabiashara pia wameelezea wasiwasi juu ya kutoweza kwao kupata pesa ambayo haina uwezekano wa kushuka kwa thamani ghafla ya kuagiza bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako