• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kusimamishwa kwa kampuni kubwa za kamare nchini Kenya kulipunguza mapato ya Safaricom

    (GMT+08:00) 2020-11-10 19:54:39

    Kusimamishwa kwa kampuni kubwa za kamare nchini Kenya kulipunguza mapato ya miezi sita ya kampuni ya mawasiliano ya Safaricom, na thamani ya shughuli kutoka sehemu hiyo ikishuka kwa asilimia 59.3.

    Matokeo ya kifedha ya kampuni ya nusu mwaka yaliyotolewa yanaonyesha thamani ya shughuli kutoka kwa kampuni za kamare imeshuka hadi Sh49.2 bilioni kutoka Sh83 bilioni ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

    Bodi ya Udhibiti na Leseni ya kamare Kenya (KBCLB) ilibatilisha leseni kwa SportPesa na Betin, ambayo ilidhibiti hadi asilimia 70 ya michezo ya kamare nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako