• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya 22 ya teknolojia za hali ya juu ya China yafanyika mjini Shenzhen

    (GMT+08:00) 2020-11-11 18:36:46

    Maonyesho ya 22 ya teknolojia za hali ya juu ya China (China Hi-Tech Fair) yamefanyika kuanzia leo hadi tarehe 15 mjini Shenzhen. Katika maonyesho hayo, nchi na mashirika ya kimataifa 24 yanashiriki moja kwa moja, na mengine 29 yakishiriki kwa njia ya mtandao.

    Naibu mkurugenzi wa kamati ya maandalizi ya maonyesho hayo ambaye pia ni naibu meya wa mji wa Shenzhen Bw. Ai Xuefeng amesema, kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu ni "teknolojia yabadilisha maisha, uvumbuzi wahimiza maendeleo", ambayo yatakukusanya rasilimali za uvumbuzi, kuhimiza muungano na maendeleo ya uzalishaji, teknolojia na mitaji, ili kufanya kazi kwa ajili ya kuinua kiwango cha uvumbuzi wa teknolojia, kuhimiza ushirikiano wa teknolojia na uchumi wa kimataifa, kuimarisha uwezo wa kukabiliana na msukosuko na kuongeza motisha wa maendeleo ya uchumi.

    Habari zinasema maonyesho hayo kwa mara ya kwanza yaliweka eneo maalumu ya huduma ya kibiashara ya 5G, na eneo la matumizi ya Tehama kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako