• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamati ya kudumu ya bunge la umma la China yapitisha uamuzi kuhusu Hong Kong

    (GMT+08:00) 2020-11-11 18:37:12

    Mkutano wa 23 wa kamati ya kudumu ya awamu ya 13 ya bunge la umma la China umefungwa leo hapa Beijing, ambapo umepitisha uamuzi kuhusu suala la sifa ya wabunge wa bunge la mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong.

    Uamuzi huo umeweka bayana kuwa wabunge wa mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong wakikutwa na kosa la kujihusisha na vitendo vya kueneza au kuunga mkono harakati ya "Hong Kong kujitenga na China", kukataa kutambua China bara kuwa na mamlaka ya Hong Kong, Kutafuta nguvu za nchi za nje kuingilia kati mambo ya Hong Kong, au vitendo vingine vinavyoharibu usalama wa taifa, watavuliwa ubunge mara moja.

    Siku hiyo hiyo serikali ya mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong imetangaza kuwavua ubunge wabunge wanne wa bunge la awamu ya sita la Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako