• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa chama cha Soka cha Uingereza aachia ngazi kwa aibu

    (GMT+08:00) 2020-11-11 18:45:39

    Mwenyekiti wa chama cha Soka cha Uingereza Greg Clarke amelazimishwa kujiuzulu kwenye nafasi yake katika mazingira ya aibu baada ya lugha yake kuwakera wabunge wa Uingereza na kuchafua sifa ya Chama hicho. Greg mwenye umri wa miaka 63 amelazimika kuachia ngazi mara tu baada ya maelezo yake ya "wanasoka wenye rangi", miongoni mwa matamshi mengine kama vile waasi wako kwenye idara ya Tehama na wale wenye asili ya Afrika na Caribbean wako uwanjani, kusababisha mshtuko na hasira katika ulimwengu wa soka. Hatua hiyo inakuja wiki chache tu baada ya FA kutaka kuchukua uongozi katika ujumuishaji wa michezo na uzinduzi wa Kanuni za Utofauti wa Uongozi wa Soka. Kufuatia mkutano wa dharura wa bodi ya FA, ilitangazwa kwamba Clarke ataondoka mara moja katika nafasi aliyoshikilia tangu 2016. Clarke pia kwa sasa ni makamu wa mwenyekiti wa Fifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako