• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Ureno wavamia ofisi za vilabu vitatu kuchunguza ukwepaji kodi kuhusu uhamisho wa wachezaji

    (GMT+08:00) 2020-11-11 18:45:56

    Polisi nchini Ureno wamevamia ofisi za klabu za ligi kuu ya nchi hiyo Benfica, Sporting na Santa Clara kama sehemu ya uchunguzi wa ufisadi na utapeli wa pesa unaohusishwa na uhamisho wa wachezaji. Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Ureno imesema karibu uchunguzi 30 ulifanywa Jumatatu na Polisi wa Mahakama na Mamlaka ya kodi chini ya uongozi wa Wizara ya Umma. Klabu zote tatu zimethibitisha kutuokea kwa tukio hilo, na Benfica imeonyesha nia kamili ya kushirikiana na mamlaka. Sporting alisema katika taarifa yake uchunguzi unahusiana na madai ya ukiukwaji wa sheria kutoka 2011-14 na kupongeza juhudi za kukuza uwazi katika soka nchini Ureno. Waendesha mashtaka wamesema wanachunguza kesi mbalimbali, zote zinahusishwa na mpira wa miguu, ambazo zinaweza kujumuisha uhalifu wa ushiriki wa kiuchumi katika biashara au kupokea faida isiyofaa, ufisadi, ulaghai wa kodi na utapeli wa pesa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako