• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwakinyo kupanda ulingoni ijumaa hiyo kujaribu bahati yake dhidi ya muargentina

    (GMT+08:00) 2020-11-11 18:46:14

    Bondia Hassan Mwakinyo ameahidi kumpiga mpinzani wake, Muargentina Jose Carlos Paz na kutetea taji lake ubingwa wa Mabara wa WBF uzito wa Super-Welter katika pambano la raundi 12 Ijumaa ukumbi wa Next Door Arena, Masaki Jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari kwenye hoteli ya Colosseum, Masaki Jijini Dar es salaam. Mwakinyo amesema atahakikisha Paz anaachana na mchezo wa ngumi za kulipwa kutokanana kipigo alichomwandalia. "Amesema anatamani pambano lifanyike mapema iwezekanavyo, hata siku moja kabla kwani yuko zaidi ya aivyokuwa mwanzoni. Amesema hataki kuwasikitisha watanzania katika pambano hilo. Alisema anajua kuwa Paz ni bondia mzuri na amejiandaa vyema katika pambano hilo, lakini kutokana na jinsi na yeye alivyojiandaa, hatakuwa na nafasi ya kutamba kwake. Bondia Paz amesema hajaenda Tanzania kutalii bali kumvua ubingwa Mwakinyo. Nitamfundisha ngumi Mwakinyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako