• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanariadha wa Kenya waendelea kung'ara kimataifa, safari hii ni Istanbul Marathon

    (GMT+08:00) 2020-11-11 18:46:33

    Wanariadha wa Kenya Bernard Cheruiyot na Diana Chemtai wametawazwa mabingwa wa Istanbul Marathon nchini Uturuki baada ya mashindano yaliyofanyika Novemba 9, 2020. Cheruiyot aliweka muda bora wa binafsi baada ya kukata utepe kwa saa 2:11:49 kwa upande wa wanaume. Alifuatwa na Mkenya Felix Kimutai (2:12:00) ambaye alimpiku Zewudu Hailu Bekele wa Ethiopia aliyepata nafasi ya tatu baada ya saa 2:12:23. Kwa upande wa wanawake Chemtai alifanikiwa kusajili muda wa saa 2:22:06 mbele ya Waethiopia Hiwot Gebrekidan (2:24:30) na Tigist Memuye (2:37:52) waliokamata nafasi za pili na tatu mtawalia. Katika mbio tofauti zilizojumuisha wanariadha wazawa wa Uturuki pekee, Yavuz Agrali alitawala kitengo cha wanaume na kuibuka mshindi wa Turkish Marathon baada ya saa 2:19:23. Tubay Erdal aliyeambulia nafasi ya sita katika mbio za jumla awali, aliibuka mshindi wa mbio za Turkish Marathon kwa upande wa wanawake baada ya saa 2:41:11.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako