• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika Kupokea dola bilioni tano za kununua chanjo

    (GMT+08:00) 2020-11-11 18:51:28

    Umoja wa Afrika unasubiri kupokea ahadi ya dola bilioni 5 zilizoahidiwa na Benki ya Dunia na wafadhili wengine ikiwa ni kati ya dola bilioni 12 ambazo nchi za Afrika zinahitaji kupata chanjo ya Covid-19 inayokuja.

    Kampuni kubwa za dawa duniani Pfizer na BioNTec zimesema tayari watu waliokuwa wanafanyiwa majaribio ya chanjo hiyo wamekuwa na ufanisi wa asilimia 90.

    Kwenye Kampuni hizo sasa zinashinikiza idhini ya matumizi ya dharura kutoka kwa Utawala wa Chakula na Dawa za Merika.

    Kwenye mkutano wa njia ya video ulioitishwa na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat alisema Afrika inahitaji chanjo karibu asilimia 60 ya idadi ya watu ili kuthibiti maambukizi ya covid-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako