• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Raia wa Uganda kuanza kutafuta ajira nje ya nchi

    (GMT+08:00) 2020-11-11 18:52:08

    Uganda imeondoa marufuku ya usafirishaji wa wafanyikazi wahamiaji baada ya kusimamishwa kwa miezi nane katika juhudi za kuzuia kuenea kwa janga la COVID-19.

    Waziri wa jinsia, kazi na maendeleo ya jamii, Frank Tumwebaze, alisema katika taarifa kwamba kampuni zote zilizo na leseni zinazohusika na kutafuta ajira za nje kwa wahamiaji wa Uganda wataanza tena oparesheni zao.

    Kuondolewa kwa marufuku hiyo kunafanyika miezi miwili baada ya Rais Yoweri Museveni mwishoni mwa Septemba kutangaza kufunguliwa kwa uwanja wa ndege wa kimataifa na mipaka ya ardhi, ambayo ilifungwa wakati janga hilo lilitokea mwezi Machi.

    Mnamo Oktoba 1 Uganda ilianza tena safari za abiria za kibiashara baada ya kusimamishwa kwa miezi saba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako