• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakulima wataka fedha zaidi kwenye bodi

    (GMT+08:00) 2020-11-11 18:52:24

    Wakulima wa mahindi eneo la Bonde la Ufa nchini Kenya wametoa wito kwa serikali kuharakisha kutoa pesa kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Nchini (NCPB) ili kuiwezesha kununua mahindi kutoka kwao.

    Wakulima hao wamekuwa wakichelea kupeleka mazao yao katika maghala ya NCPB kwa sababu bodi hiyo haina hela za kuwalipa.Walitoa wito kwa serikali kuharakisha utekelezaji wa kanuni kuhusu mfumo wa Upokezi wa Mabohari ili kuhakikisha wakulima wananufaika kutokana na zao hilo.

    Aidha, wametoa wito kwa serikali kuu na za kaunti kusaidia vyama vya mashirika kupata mitambo ya kukaushia nafaka inayoweza kwenda maeneo mbalimbali ili kuwawezesha kudhibiti hasara msimu huu kutokana na mvua inayoendelea kunyesha.

    Zao hilo linauzwa kati ya Sh1, 700 na Sh2, 300 kwa kila gunia ya kilo 90.Bw Elijah Bett, mkulima wa mahindi kutoka eneo la Soy, Kaunti ya Uasin Gishu, alisema serikali ni sharti inunue mahindi kwa Sh3,000 kwa kila gunia la kilo 90 ili kuwawezesha kupata faida kutokana na gharama kuu ya uzalishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako