• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uuzaji bidhaa wa Kenya kwa nchi za Afrika waongezekana kufikia kiwango cha kabla ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-11-12 09:18:13

    Benki kuu ya Kenya CBK jana ilisema kuwa, uuzaji bidhaa wa Kenya kwa nchi za Afrika umeongezeka na kufikia kiwango cha kabla ya COVID-19, ambapo inaonekana janga hili linahimiza biashara kati ya Kenya na nchi za nje.

    Kulingana na data za usafirishaji zilizotolewa na Benki Kuu ya Kenya, bidhaa za nchi hiyo zilisafirishwa katika nchi za Uganda, Tanzania, Rwanda, Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Uganda ni soko la kwanza kwa kununua bidhaa za Kenya zenye thamani ya dola milioni 73.6 kwa mwezi, ikifuatiwa na Tanzania iliyoagiza bidhaa za dola milioni 24.2 kwa wastani wa mwezi.

    Uuzaji bidhaa wa Kenya kwa nchi za nje uliongezeka kuanzia mwezi Aprili na kufikia shilingi bilioni 22.5 za Kenya, ambazo ni sawa na dola za kimarekani milioni 208 mwezi Agosti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako