• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping kuhudhuria mikutano ya kimataifa kwa njia ya video

    (GMT+08:00) 2020-11-12 10:04:31

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, kutokana na mwaliko wa rais Vladimir Putin wa Russia, rais Xi Jinping wa China atahuduria mkutano wa kilele wa nchi za BRICKS tarehe 17 Novemba. Na kutokana na mwaliko wa waziri mkuu Muhyiddin Yassin wa Malaysia, rais Xi atahudhuria mkutano usio rasmi wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki utakaofanyika Novemba 20. Vile vile kwa mwaliko wa mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia, rais Xi Jinping atashiriki kwenye mkutano wa kilele wa Kundi la nchi 20 utakaofanyika Novemba 21 hadi 22. Mikutano hiyo itafanyika kwa njia ya video.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako