• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kesho Taifa stars inashuka dimbani kutupa karata ya kwanza AFCON

    (GMT+08:00) 2020-11-12 18:51:33

    Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Etienne Ndayiragije, amesema kuwa kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya wana imani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kufuzu Afcon kesho, Novemba 13. Stars iliweka kambi ya muda wa siku tatu nchini Uturuki ikiwa ni maandalizi ya mchezo huo wa kesho ambao utachezwa bila ya uwepo wa mashabiki kutokana na Shirikisho la Soka Afrika,(Caf) kutaka iwe hivyo ili kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona. Utachezwa Uwanja wa Olympique de Rades nchini Tunisia na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Novemba 17, Uwanja wa Mkapa na umeruhisiwa kuwa na nusu ya mashabiki na Caf wenyewe. Ndayiragije kwenye mchezo wa kesho atawakosa washambuliaji wawili ambao ni pamoja na Adam Adam yeye ni mzawa alikosa paspoti ya kusafiria pamoja na Mbwana Samatta ambaye anasumbuliwa na maumivu ya msuli. Stars ipo kundi J ina pointi tatu ikiwa inakutana na Tunisia ambao ni vinara wakiwa na pointi sita hivyo ikishinda itaongeza nafasi ya kunusa hatua ya kufuzu Afcon 2021 nchini Cameroon.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako