Timu ya Taifa ya Tanzania, chini ya miaka 20 leo Novemba 11 imekubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Sudan. Mchezo wa leo wa kirafiki umechezwa Uwanja wa Uhuru ambapo Sudan ilianza kufunga bao la kwanza dakika ya 10 kupitia kwa Mustafa Hassan dakika ya 10 na lile la pili lilifungwa na Nagigouma Alamin dakika ya 56. Bao la kufutia machozi kwa Tanzania lilifungwa na Tepsi Evans dakika ya 63 na lilidumu mpaka dakika 90 zilipokamilika. Nahodha wa timu ya Tanzania, Kelvin John amesema kuwa wameshindwa kutumia nafasi ambazo wamezipata jambo ambalo limewaadhibu. Amesema mchezo ulikuwa mzuri na wenye ushindani, wenzao walitumia makosa yao na kupata ushindi huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |