• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaanza vibaya safari ya kutaka kucheza AFCON 2022

    (GMT+08:00) 2020-11-12 18:52:11

    Mechi ya kwanza ya Harambee chini ya kocha Jacob Mulee imekuwa ya kusikitisha kiasi baada ya wenyeji kutoka sare ya bao 1-1 na Comoro, ambao walijikuta wakibaki wachezaji 10 uwanjani, katika mchezo uliochezwa jana katika uwanja wa kasarani. Youssef M'Changama alikuwa wa kwanza kuwafuruhisha wageni katika dakika ya 26 kwa free kick moja nzuri. Hata hivyo ni yeye mwenyewe alibadilika kuwaumiza wenzake baada ya kupewa kadi ya pili ya njano na kutolewa uwanjani akiwaacha wenzake 10 kupambana na Harambee stars dakika tano kabla ya half time. Kenya ilitumia faida yao katika kipindi cha pili na Masud Juma aliunganisha bao la kusawazisha dakika ya 65. Comorro hawakuwa wepesi kama ilivyodhaniwa, na wanaweza kufanya maajabu kwenye mechi ya marudiano itakayochezwa jumapili huko Moroni. Kwa sasa Comoro inaongoza kundi lake kwa kuwa na pointi tano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako