• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mataifa ya EAC kuunda mfumo wa pamoja wa ushuru wa kidijitali

    (GMT+08:00) 2020-11-12 18:56:49

    Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimeamua kuja na mkakati wa pamoja wa ushuru wa kidijitali.

    Hayo yaliafikiwa jana katika mkutano ulioandaliwa kwa njia ya video.

    Viongozi wa Mamlaka za Mapato kutoka nchi saba wamekubaliana kwamba sera hiyo itasaidia ,kwa sababu itarekebisha masuala ya mfumo wa kisheria kama vile kutambua wadau katika sekta hiyo pamoja na taratibu za kisheria.

    Mkutano huo ulijadili masuala ibuka ambayo yanaendelea kuathiri tawala za ushuru na kukubaliana kuunda mkakati wa pamoja kwa ajili ya Mamlaka za Mapato za Afrika Mashariki kushughulikia ushuru wa kidijitali.

    Mkutano huo ulihudhuriwa na Audace Niyonzima (Burundi), Pascal Ruganintwali (Rwanda), Patrick Mugoya (Sudan Kusini), Alfred Mregi (Tanzania), John R. Musinguzi (Uganda), Joseph A. Meza (Zanzibar) na Githii Mburu (Kenya)

    Azimio hilo linakuja siku kadhaa baada ya Mamlaka ya Mapato ya Kenya kutangaza kuwa itaanza kutoza ushuru miamala ya mtandaoni kuanzia mwezi Januari 2021.

    Viongozi hao wa tawala za ushuru pia walikubaliana kuishirikisha Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu umuhimu wa kuanzisha kamati ya masuala ya ushuru,sehemu ambayo masuala yanayohusiana na ushuru na masuala mengine ya utawala yasiyohusiana na forodha yanaweza kushughulikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako