Wenye viwanda wa ndani nchini Rwanda wanalenga ufunguzi wa shule kama soko ambalo wataingiza barakoa zaidi ya milioni 2.7 ambazo bado zipo kwenye mabohari.
Wenye viwanda wa ndani wasiopungua 40 walikuwa na mali ya zaidi ya barakoa milioni 3 mwezi Agosti 2020.Barakoa hizo zilitengezwa hadi mwezi Juni,lakini hazikupata soko kutokana na muundo usiopendeza ambao haukupendelewa sana na wateja.
Ili kushughulikia suala hili,serikali ya Rwanda ilianzisha kampeni ya barakoa kwa watu wote,ambayo ililenga kushughulikia changamoto hiyo kwa kuwaleta pamoja wadau wote wa sekta binafsi na umma kuchangia katika kununua na kusambaza barakoa kwa wafanyakazi wao.
Hata hivyo,Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Mask Investment Limited,Swaib Munyawera,anasema kuwa wadau wote waliowaendea ili kununua barakoa hizo walisema wameathiriwa mno na janga la corona hivyo hawakuwa na uwezo wa kuzinunua.
Munyaweara anaongeza kuwa katia ya barakoa milioni 3 zilizokuwa kwenye mabohari kufikia mwezi Agosti 2020,ni 300,000 zilizouzwa kupitia kampeni hiyo.
Wizara ya Biashara na Viwanda nchini humo imeamua kushughulikia suala hilo kupitia wanafunzi ambao wanarudi shuleni.
Mkurugenzi Mkuu wa Viwanda katika Wizara ya Biashara na Viwanda nchini Rwanda,Sam Kamugisha, amesema kuwa wamefanya mkutano wa mashauriano na Wizara ya Elimu ili kutafuta njia ya kuuza barakoa kwa wanafunzi shuleni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |